Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wiki mbili kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa wilaya ya Mkuranga na Mkurugenzi Mtendaji wake wahakikishe shule za msingi na sekondari za Mwarusembe zinakuwa na madawati.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 13, 2020 wakati akizungumza na wananfunzi na walimu wa shule ya msingi Mwarusembe mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika shule hiyo na kukuta baadhi ya wanafunzi wamekaa chini.

“Nataka Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri na wakuu wa idara hasa wa elimu mjipange upya katika suala la madawati. Nikija tena na nisipokuta madawati, mjiandae” amesema Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema ukosefu wa madawati unawafanya walimu washindwe kusimamia usafi kwa wanafunzi lakini pia amesema wazazi wanaingia Gharama kununua sabuni ili watoto wao wafue nguo kila siku.

Uganda: Kiongozi wa upinzani akataa kugombea urais 2021
Ujerumani mambo magumu, Ligi Kuchezwa bila mashabiki