Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imesema itaanzisha kilimo cha korosho kama zao mbadala la biashara litakaloungana na lile la tumbaku ikiwa ni hatua ya kuandaa malighafi kwa ajili ya viwanda,

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,  Simon Ngatunga wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambapo amesema tayari ameshawaandikia barua Bodi ya Korosho nchini kwaajili ya kupatiwa miche ya mikorosho.

Amesema kuwa udongo wa Sikonge unafaa kwa ajili ya zao la Korosho jambo ambalo linatoa fursa nyingine kwa wakazi wa Sikonge kuwa na zao jingine linaloweza kuwapatia fedha.

Aidha, kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi wote katika halmashauri zote nane mkoani humo kuhakikisha wanasisitiza kilimo cha korosho, Alizeti na Pamba kwa Wilaya ya Urambo, Igunga , Kaliua ,Nzega na Uyui.

Hata hivyo, Mwanri amesisitiza kuwa ardhi ya Tabora inakubali mazao mbalimbali na hivyo wanataka kutumia fursa hiyo ya uzuri wa ardhi kumwongezea mkulima wigo wa mapato na kwa upande mwingine kuziongezea Halmashauri mapato ya ndani.

 

Ligi ya wanawake kuanza na ligi ndogo
Sekunde 14 zaiponza Leicester City