Muigizaji wa Marekani Will Smith amejiuzulu kutoka Taasisi ya Oscars siku chache baada ya kumpiga kibao mchekeshaji Chris Rock jukwaani wakati wa utolewaji wa tuzo za Oscar Machi 28, 2022 katika ukumbi wa Dolby huko Los Angeles. .

Kwa mujibu wa Smith amesema kuwa “Matendo yangu katika utoaji wa Tuzo za 94 za Academy yalikuwa ya kushtua, ya kuumiza, na hayana utetezi”.

Taasisi Y Oscar imesema kuwa imekubali kujiuzulu kwake na itaendelea kusonga mbele na taratibu za kinidhamu.

Itakumbukwa Muigizaji Smith alimpiga Rock kwasababu ya mzaha kuhusu kichwa kilichonyolewa cha mke wake, matokeo ya hali ya upotezaji wa nywele.

Chini ya saa moja baadaye, alitunukiwa tuzo ya mwigizaji bora kwa jukumu lake katika “King Richard”, ambapo alicheza baba wa nyota wa tenisi Venus na Serena Williams.

Mathias Lule: Wachezaji wangu wamejisahau
TRA kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki kuanzia mwezi huu