Muigizaji kutoka Marekani, Will Smith amemuomba radhi mchekeshaji Chris Rock pamoja na waandaji wa tuzo za Oscar baada ya kumchapa kofi mchekeshaji huyo akiwa jukwaani wakati wa utolewaji wa tuzo za 94, usiku wa kuamkia Machi 28, 2022.

Licha ya kuomba radhi akiwa jukwaani muda mfupi baada ya tukio na kushinda tuzo, Will ameamua kuutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram wenye jumla ya wafuasi milioni 61.8, kuomba radhi tena kufuatia kitendo hicho kilichozua gumzo kubwa kote duniani.

“Vurugu katika aina zake zote ni sumu na uharibifu. Tabia yangu katika tuzo Jana usiku haikukubalika na haina udhuru. Utani ni sehemu ya kazi, lakini mzaha kuhusu hali ya kiafya ya Jada ulikuwa mzito sana kwangu na niliitikia kihisia, Aliandika Will.

Ameongeza, “Ningependa kukuomba msamaha hadharani, Chris, Nilikuwa nje ya mstari na nilikosea Nina aibu na matendo yangu hayakuwa dalili ya mwanaume ninayetaka kuwa, Hakuna mahali pa jeuri katika ulimwengu wa upendo na fadhili,”

Pia ningependa kuomba radhi kwa Academy, watayarishaji wa kipindi, wahudhuriaji wote na kila mtu anayetazama duniani kote, ningependa kutoa pole kwa familia ya Williams na familia yangu ya Mfalme Richard, Ninajuta sana kwamba tabia yangu imenichafua.” Ameandika Will Smith.

Katika tukio hilo Will Smith alikasirishwa na kitendo cha Chris kumtania mke wake Jada kwa utani ambao umeendana na tatizo lake la kiafya.

Haji Manara: Fiston Mayele hauzwi
Lita yatakiwa kuwa chanzo Cha elimu bora ya mifugo