Moja ya vitu vinavyoonyesha kukua kwa mziki wa bongo fleva ni kutumika katika matamasha na shughuli mbalimbali hasa nje ya nchi, miongoni mwa wasanii ambao nyimbo zao huchezwa nje ya nchi hasa bara la Ulaya na Marekanini ni Diamond Plutnumz, Vanessa Mdee na Alikiba.
Vanessa Mdee anaetamba na wimbo wa ‘That for me’ ameshea video ambayo wimbo huo umesikika kwenye spika za uwanja wa American airlines center mjini Dallas Texas ambapo mchezo wa kikapu NBA kati ya Dallas Maverricks na New Orleans pelicans ulipigwa alfajiri ya kuamkia jana na Orleans kuibuka na ushindi wa vikapu 129-125.
Aidha, Vanessa alipata shavu la kufanya kazi na moja ya record lebal kubwa duniani Universal Music Group huku wimbo huo wa That for me aliowashilikisha wakali kutoka Afrika Kusini Djtira, Distruction, Boyz na Princebulo kazi hiyo ilifanyika chini ya record lebal hiyo.
Mwanamuziki huyo wa bongo fleva anaendelea kuwakilisha vyema Tanzania katika sekta tofauti ambapo pia alishiliki kwenye mkutano mkubwa akiwakilisha wanawake wa Afrika na vijana wa kitanzania hususani watoto wa kike kwenye Cransmontanaforum iliyofanyika Dakhla Morocco.
Aidha mziki wabongo fleva umekuwa chachu katika kukuza vipaji na kutangaza nchi ya Tanzania kimataifa huku wasanii wengi wakipata nafasi ya kuwakilisha nchi na kutangaza lugha ya kiswahili katika mataifa mengine.