Uongozi wa klabu ya AS Roma ya nchini Italia, umemkana mshambuliaji kutoka Bosnia & Herzegovina, Edin Dzeko ambaye ameripotiwa kuwa katika mipango ya kuondoka mjini Manchester, Uingereza kuelekea mjini Roma, Italia.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya AS Roma, Walter Sabatini, hivi karibuni alikanusha taarifa hizo kwa kusema hakuna mpango wowote za usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Sabatini, aliamua kukanusha taarifa hizo, baada ya kudaiwa kuwa uongozi wa Man City, umeitaka AS Roma kuongeza dau mara mbili la paund milioni 20 ili kuweza kumpata Dzeko ambaye imeonekana hatokua na nafasi katika kikosi cha kwanza kuanzia msimu ujao wa ligi.

Kabla ya kuibuka kwa madai hayo Man City walitangaza ada ya uhamisho wa Eden Dzeko kuwa ni paund milioni 49.

Mipango ya usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Uingereza, Raheem Sterling huko Etihad Stadium, imekuwa kichocheo kikubwa kwa Dzeko kufunguliwa milango la kupewa uhuru wa kuchagua popote anapotaka kwenda kusaka rizki yake ya kila siku.

Mastaa Wa Marekani Wamuimbia Tajiri Wa ‘Unga’ Aliyetoroka Jela, ‘El Chapo’, Sikiliza Hapa
Fabio Capello Akubali Kubwaga Manyanga Urusi