Mkutano wa kilele wa kuunganisha vijana umemalizika jijini Kigali, nchini Rwanda baada ya siku 3 za makongamano, mafunzo bora na vipindi vya mitandao ukiwakutanisha maelfu ya wabunifu vijana na viongozi kutoka kote ulimwenguni waliohudhuria na kujadili njia tofauti za ukuaji na maendeleo kwa vijana wa bara la Afrika.
Mkutano huo, wa kilele wa mwaka huu (2022), ulikuwa unafanyika chini ya mada inayosema “Kuongeza kasi ya uwekezaji kwa Vijana: Vijana Resilient, Afrika Resilient” ikiwakutanisha washiriki kutoka nchi 30 za Afrika ambapo pia ulijadili jinsi ya kuwashirikisha vijana katika biashara ya Afrika, afya, ustahimilivu wa hali ya hewa na ufadhili, teknolojia na ujuzi kwa siku zijazo.
Hata hivyo, kulingana na matokeo ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), asilimia 42 ya Vijana barani Afrika hawawezi kupata ufadhili unaohitajika kuendesha biashara zao, na wakati mwingine mawazo yao hubaki bila kuyafanyia kazi na kushindwa kufanikisha ndoto zao.
Wajumbe wa ngazi ya juu akiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame walisisitiza kuwa vijana ni vuguvugu dhabiti ambalo litachangia ajenda ya mafanikio ya 2063 kwa Afrika bora ambapo ajenda kuu ya Umoja wa Afrika (AU), ya mwaka 2063 ni mfumo wa bora unaolenga kufikia malengo ya maendeleo jumuishi.