Jeshi la Polisi nchini limesema asilimia kubwa ya mauaji yanayotokea hapa nchini yanatokana na wivu wa mapenzi na Wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Kwenye Ripoti yake ya mwaka 2020, Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya mauaji, limewataka Viongozi wa Dini kuingilia kati na kutoa Elimu ili kupunguza vifo hivyo kwani wengi ni Waumini wao na wanawasikiliza.
Aidha, matukio mengine ambayo yamejitokeza mwaka huu tofauti na miaka ya nyuma, ni pamoja na unyang’aji wa kutumia silaha, ajali za barabarani, Shule kuungua moto na wanafunzi kuacha masomo ili kujiunga na makundi ya kihalifu.
Jeshi lla Polisi pia limewaomba wazazi kuwafuatilia watoto wao likisema, wapo wanafunzi ambao wamekamatwa wakivuka mpaka kuelekea Msumbiji na wengine tayari wamefanikiwa kufika nchini humo.