Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais, (TAMISEMI), kuandaa utaratibu utakaosaidia vijana kujifunza na kufahamu historia ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Majaliwa ametoa maagizo hayo wqkati wa kongamano la kumbukizi ya miaka 101 kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere, lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kufanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM.

Amesema, yapo mambo ambayo Vijana wanapaswa kuyajua ikiwemo kumfahamu na kumuelezea Baba wa Taifa, na hasa kipaji chake katika harakati za kupigania uhuru, kutambua juhudi na harakati za kuleta amani, kuimarisha ustawi wa Tanzania na maisha yake kiujumla.

Aidha, ameongeza kuwa wakati wa uhai wa Mwalimu kwenye uongozi wake alisisitiza suala la urithi na falsafa zake, kupinga ukabila na kukemea udini ikiwemo kuwaasa watu kutotafuta uongozi kwa misingi ya udini.

“Tusiingie huko kwenye masuala ya ukabila na udini, jambo jingine kupambana na ujinga, maradhi na umasikini, maadili ya uongozi na kupinga rushwa, alisisitiza Mwalimu viongozi safi wasiopenda rushwa na rushwa ndio adui wa maendeleo yetu,” ameongeza Majaliwa.

Hata hivyo, amesema katika harakati za kisiasa Mwalimu alitamani kuunganisha nchi na kuwa na uongozi wa pamoja, jambo ambalo lingeleta mafanikio ya nchi.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda alihuhudia kuwahi kutumikia Ofisi binafsi ya Mwalimu Nyerere, kutokana na uzalendo na nidhamu ya maisha.

Mwenge wa Uhuru 2023 wapiga hodi mkoani Morogoro
Charles III rasmi sasa ni Mfalme wa Uingereza