Naibu waziri wa afya Faustine Ndugulile Amesema miaka 50 ijayo wanaume watakuwa hawana nguvu za kiume kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi vyakula wanavyokula ikiwemo ”chips”.

Ndugulile ametoa kauli hiyo wakati wa kujibu hoja zilizojitokeza katika kikao cha kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii alipokutana na wizara hiyo na taasisi zake, amesema tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kwa miaka 50 kumekuwa na upungufu wa nguvu za kiume kwa asilimia 50.

Katika hatua nyingine amesema kuwa huduma ya ugumba imekuwa tatizo kubwa sana nchini na kwasasa hospitali ya taifa ya Muhimbili imeshaanza mandalizi ya kuanzisha huduma hiyo.

”Tunatambua hospitali binafsi zinafanyia kazi jambo hili ,tunaka kwa upande wa seriiakali na sisi tuanzae kutoa huduma”amesema

Naye mbunge wa viti maalumu( Chdema) Susan Lyimo ameishauri serikali ya Tanzania kutoa elimu ya sababu ya wanaume kutokuwa na mbegu zenye nguvu ili kunusuru ndoa.

Amesema kwa sababu ya mfumo dume  walikuwa wanasema mwanamke ndiye mwenye tatizo lakini sasaivi tatizo hilo limegeukia kwa wanaume.

” Wanaume nao wakubali kwasasabu nao wana tatizo, mimi nilikuwa nadhani kuna haja ya kutoa elimu toeni ninisababu za wanaume kutokuwa na mbegu zisizokuwa na nguvu ili wake zao au wanawake zao wapate watoto”amesema Lyimo.

Laini za simu kuzimwa kwa awamu
Prof. Lipumba kuandika barua kwa Magufuli, msafara wake wazuiwa

Comments

comments