Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imemsafirisha mtoto, Antonia Justine Msoka anayeongezeka uzito kila kukicha kwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 17 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili tangu Novemba mwaka jana na kuanza kupatiwa matibabu.
“Nashukuru kwa msaada kwani sasa naenda Hospitali ya India kwa matibabu zaidi, naishukuru pia serikali kwa kunisadia,” amesema Antonia.
Awali mtoto huyo alifikishwa Muhimbili akiwa na uzito wa Kilo 250, lakini sasa zimepungua na kufikia kilo 230
Kwa upande wake Mama wa mtoto huyo,Salome Manyirizu Kisusi ameishukuru wizara ya Afya kwa msaada fedha za matibabu na kumsafirisha kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi

Mourinho kuvuta majembe mapya Manchester United
Video: Chenge, Werema wajivua lawama, Acacia waomba tume huru, uchunguzi mpya