Wizara ya afya imetoa kondomu 3,000 kwa waathiriwa wa mafuriko zaidi ya 6,000 walioko katika kambi katika Shule ya Garashi, kaunti ya Kilifi.
Kwenye taarifa ya vyombo vya habari ,Waziri wa Afya Dkt. Anisa Omari amesema kuwa mbali na kondomu hizo wamezidisha huduma za afya kwa waathiriwa wote walioko kambi ya Garashi.
‘’Tumepeleka Kondomu 3,000 kwa waathiriwa hao walioomba wapewe. mbali na mipira hiyo tumeweka kliniki katika mojawapo ya madara katika shule hiyo’’amesema Dkt. Omari na kuongeza kwamba
Hata hivyo amesema kuwa wamepeleka wafanyakazi wanaotoa huduma za afya mchana na usiku, na kuongeza kuwa wataendelea kuwahudumia wakazi hao mpaka hali itakapoimarika na warudi makwao, ’’amesema Dkt. Omari
Wananchi hao zaidi ya 6,000 walioathiriwa na mafuriko katika eneo la Malindi waliomba kusambaziwa mipira hiyo ili kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwamo ukimwi.
Wakizungumza na waandishi wa habari wamesema kwamba kwa sababu wako wengi kuna vijana ambao bado damu zinachemka,kuna hatari miongoni mwao kuanza kufanya mapenzi na hivyo basi kuzua hofu ya kupata magonjwa.
“’Tunahitaji kuletewa mipira ya kondomu kwa sababu tumekuwa wengi hapa na hatujui wengine wako na hali gani.Pengine umekutana na mtu wako ambaye mlikuwa mkiendelea naye huko nje. Sasa ni balaa.Ni afadhali ziletwe kwa wingi ziweze kusaidia.Yote ni mambo na afya tu,’’amesema mwanamke mmoja ndani ya kambi hiyo.
Aliyemuua mpenzi wake na kumchoma anasa mahakamani