Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imetoa zawadi ya Sikuu ya Krismasi yenye thamani ya shilingi 280,000 kwa wazee waishio katika Makao ya Taifa ya Wazee Sukamahela Wilayani Manyoni Mkoa wa Singida kama sehemu ya kuenzi mchango wao kwa Taifa.
Akitoa zawadi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto Wizarani hapo, Sebastian Kitiku amewaambia wazee hao kuwa serikali inathamini mchango wa wazee katika ujenzi wa Taifa.
Amesema kuwa pamoja na zawadi hiyo ya Krismasi Wizara pia inawahakikishia wazee hao kuwa itamaliza changamoto zote zinazowakabili wazee hao ili waweze kuishi katika mazingira safi na salama.
‘’Nawapa nafasi wazee kuongea na sisi ili tuweze kujua changamoto mlizonazo ili Wizara iweze kuwasikiliza na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kuweka mazingira rafiki na salama katika makao haya.’’ Amesema Kitiku.
Aidha moja ya changamoto inayowakabili kwenye makao hayo ya Wazee Sukamahela ni ukosefu wa nishati ya umeme jambo lilinalosababisha wazee hao kuishi katika mazingira magumu hasa nyakati za usiku hivyo wazee hao kwa pamoja wameiomba Wizara kutatua chanagamoto hiyo.
-
Ole wake kiongozi wa dini atakaye hubiri Siasa- Lugola
-
Makonda afuta likizo kwa wakuu wa idara za afya
-
Umoja wa wabangua Korosho wampongeza JPM
Hata hivyo, wizara imeahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo ili wazee hao waweze kuishi katika mazingira safi na salama kwa kuwa serikali inawathamini, kuwapenda na kutambua mchango wao hususani mchango wao katika maendeleo ya Taifa.