Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa siku 60 kuanzia tarehe 5 Februari, 2022 kuhakikisha wamiliki wa ardhi waliopimiwa viwanja wanawasilisha maombi ya kumilikishwa ardhi huku wale wenye miliki za ardhi wawe wamelipa kodi ya pango la ardhi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi ameyaeleza hayo leo Februari 4, 2022

kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Amesema, mmiliki ambaye hatalipa kodi ndani ya muda uliotolewa, Serikali itachukua hatua za kisheria ikiwemo kufuta miliki, kupiga mnada na kumilikisha viwanja vilivyopimwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji.

Ismail Rage apaza sauti kusua kwa Simba SC
Diego Costa asaka timu Ulaya