Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Serikali imefungua milango ya majadiliano na wanahabari kuhusu changamoto zao.
Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambapo ameweka wazi kwamba Serikali imetoa haki ya kupelekwa mahakamani mashauri mbalimbali kuhusiana na sheria ambazo zimepitishwa lakini bado kuna fursa nzuri ya kufanya mazungumzo na wadau.
“Serikali itaendelea kusimamia sheria zilizotungwa katika kuhakikisha wanahabari na wamiliki wa mitandao ya kijamii wanafanyakazi kwa weledi na kujali maslahi ya taifa na tamaduni,”amesema Dkt. Mwakyembe
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali itahakikisha inasimamia kuundwa kwa vyombo vitatu katika kutekeleza sheria ya huduma za habari, ambavyo ni baraza huru la habari, Bodi ya Ithibati na kuwepo kwa mfuko wa kusaidia wanahabari.
-
Video: Wabunge CCM wataka mishahara iongezwe, JPM awapasha wabunge
-
Ndalichako aagiza Nacte na TCU kuvifungia vyuo visivyokidhi vigezo
-
Waziri akemea upimaji holela wa DNA