Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa Wizara imemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kubadili sheria na kila mtu aweze kujipima Ukimwi nyumbani.

Ameyasema hayo hii leo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambulie (CUF), Masoud Abdalla Salim ambaye alitaka kujua mkakati wa ziada wa Serikali kutambua wanaopata athari za Ukimwi.

Amesema kuwa ni kweli maambukizi yameongezeka kwa mkoa wa Dodoma kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 5 sawa sawa na mkoa wa Tanga na Mwanza.

“Tunafanya utafiti maalumu kubaini kwa nini maambukizi yamepanda. tumekuwa na changamoto ya kuwapata wanaume kupima na njia ya mtu kujipima mwenyewe, na dawa za VVU zipo kwa asilimia 100,”amesema Ummy Mwalimu.

 

Fahamu mambo 5 juu ya urembo hapo kale
Watumiaji mitandao ya kijamii kulipishwa kodi kupunguza umbea