Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolijia, imekanusha juu ya taarifa ya upotoshaji inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha chapisho la kitabu lililokosewa likionesha viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu.

Ambapo katika chapisho hilo kumekuwa na makosa makubwa yalifanyika katika kuonesha sehemu za mwili huo, Wizara imesema chapisho la kitabu hiko si miongoni mwa vitabu vilivyosambazwa mashuleni kwa ajili yakufundishia na wala kitabu hiko hakifanani kabisa na vitabu vilivyochapishwa hivi karibuni na TET.

Hivyo Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imewasihi wananchi kupuuzia taarifa ambazo sio za kweli kuhusiana na chapisho la kitabu hiko, kwani ni taarifa ambazo zinapotosha jamii na kuleta mkanganyiko.

Pia imewataka watu kutumia vizuri vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii na kukumbusha kuwa kutoa taarifa za uongo ni kosa la jinai.

 

 

BBC, VOA zafungiwa miezi sita
Video: Mtoto apata ugonjwa wa ajabu