Mkuu wa Moa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesema amebaini wizi wa mafuta uanofanywa na wananchi Kigamboni ambapo mpaak sasa Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumia 15 huku uchunguzi ukiendelea.
Amesema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo ameeleza kilichomsukuma kufanya ziara hiyo kuwa ni malalamiko ya wafanyabiashara wanaoingiza mafuta kupewa mafuta punguzfu na yale waliyoagiza.
”Upo wizi na upotevu wa mafuta maana yanapopita kwenye flow meter na kwenda kwa wateja tumeshuhudia namna watu ambavyo wameweza kuingilia miundombinu hiyo kujiunganishia mabomba katikati na kujipatia mafuta hayo” amesema RC Makalla
Hatahivyo katika ziara hiyo rc Makalla ameongozana na Viongozi wa kamati ya ulinzi na Usalama akiwemo kamanda wa Polisi Dar Es Salaam Muliro Jumanne Murolo, Mkuu wa wilaya ya kigamboni Sara Msafiri.