Mwanamuziki Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu Wizkid kutoka nchini Nigeria, amefanikiwa kutajwa kuwania tuzo za Grammy mwaka 2022, kwenye takribani vipengele viwili vya tuzo hizo zenye heshima kubwa Duniani.
Wizkid ameingia kwenye kuwania kipengele cha ‘Best Global Music Perfomance’ kupitia wimbo wake ‘Essence’ aliomshirikishaTems, ambapo kipengele kingine ni ‘Best Global Music Album’ kupitia ‘Made In Lagos’ album.
Licha ya kuwa na tuzo ya Grammy aliyoichukua mapema mwaka jana kupitia wimbo alioshirikishwa na msanii kutoka nchini Marekani ‘Beyonce’, “Brown Skin Girl” .
awamu hii inaingia kwenye rekodi ya kuwa mara ya kwanza kwa Wizkid kutajwa kwenye ‘mainstream category’ akiingia na kazi zake mwenyewe,ukiachilia mbali kutajwa kama msanii aliyeshirikishwa kwenye nyimbo za wasanii wenginie kama Beyonce na Dizz Drake kwenye album yake ‘Views’ mnamo mwaka 2016.
Wasanii wengine kadhaa kutoka Afrika ambao wametajwa kwenye tuzo hizo ni pamoja Burna Boy, Femi Kuti na Angelique Kidjo wote wakichuana kwenye vipengele hivyo.
Tuzo za Grammy mwaka 2022 zitakuwa za 64 k tangu kuanzishwa kwake Mei 4, mwaka 1959, na zitafanyika Januari 31, 2022 katika ukumbi wa Staples Center huko Los Angeles Marekani.