Kina Mama wanaojifungua Katika Wodi ya wazazi Katika Hospital ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wanalazimika kulala wazazi wawili kwenye kitanda kimoja chenye futi mbili na nusu kutokana na kuzidiwa na wagonjwa.
Hayo yamesemwa na Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Hamza Mkingule alipokuwa akitoa taarifa mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Laula Ngozi katika ziara yake aliyoifanya wilayani humo kwa lengo la kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Amesema kuwa hospitali hiyo iliyojengwa miaka 40 iliyopita inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa miundombinu kama jengo la utawala, Wodi ya kijifungulia kina mama kuzidiwa na wagonjwa na ukosefu wa uzio wa hospital.
“Katika hospitali yetu tunakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa jengo la utawala, kwasasa tunatumia vyumba vya kutibia Kama ofisi, kitu kinachopelekea vyumba vya madaktari kuwa vichache ambapo Daktari wawili hukaa kwenye chumba kimoja na kupelekea wagonjwa kukosa usiri Katika kujieleza,”amesema Dkt Mkingule.
Kwa upande wake Mjumbe wa halmashauri kuu ya (CCM), Laula Ngozi amesema kuwa kama mlezi wa chama na Serikali ya mkoa wa Dodoma amezichukua changamoto hizo na kuzifikisha kwa uongozi hasa Wizara ya Afya Jinsia Wazee na Watoto ili kuweza kutatua kero hizo.
-
Dkt. Hawasi apokea wanachama wapya zaidi ya 115
-
Mwigulu Nchemba ataja chanzo cha ajali aliyoipata
-
Mwili wangu umechanwa chanwa vibaya mno- Tundu Lissu
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa, George Chigwie amesema kuwa ni lazima wanachama hao wajipange katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.