Aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa klabu ya Arsenal, Wojciech Szczesny amethibisha kuondoka kwenye klabu hiyo kwa mkopo na hii leo anatarajia kusaini mkataba wa kuitumikia klabu ya AS Roma ya nchini Italia.

Szczesny, alifikisha ujumbe wa kuondoka kaskazini mwa jijini London kwa mashabiki wake, kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Instagram jana jioni, baada ya kuweka picha ya video.

Picha hiyo alionekana Szczesny, akisema anatarajia kusaini mkataba wa mkopo hii leo na klabu ya AS Roma na aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kumpokea kwa mikono miwiwli.

Mlinda mlango huyo kutoka nchini Poland anaondoka Emirates Stadium kwa mktaba wa mkopo wa muda mrefu, kufuatia kusajiliwa kwa kipa kutoka jamuhuri ya Czech, Petr Cech.

Katika ujumbe wa picha ya televisheni aliyoiweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Szczesny alianza kwa kusema, “Habari za jioni mashabiki wa AS Roma. Nina furaha ya kutarajia kusaini mkataba na klabu yenu hapo kesho (leo) Ciao (kwa herini)!”

Szczesny anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Arsenal mwanzoni mwa msimu ujao.

Sergio Romero Rasmi Man Utd
‘Wanasiasa Hawa…WOTE MANZI GA NYANZA’