Nyota wa filamu Jacqueline Wolper amewatupia lawama watayarishaji na waongozaji wa filamu kuwa ndio wanaoharibu kazi za sanaa ya uigizaji kwani wengi wao wanahitaji warembo ambao hawana vipaji.

Amesema waongozaji wanataka warembo wawatumie kingono halafu ndio wawape kazi hata kama hawana uwezo katika tasnia ya uigizaji.

”Sanaa imekuwa shida wahusika wanataka rushwa ya ngono halafu ndio wawape majukumu  kama mtu amechukuliwa kwaajili ya urembo na sanaa yake haijulikani hawezi kuendelea”alisema Wolper

Staa huyo amedai kuwa wanawake ambo wanaingia kwenye tasnia ya uigizaji bila kipaji cha kuigiza huwa wanaishia kutumika kingono na waandaaji wa filamu, ameongeza kuwa hawezi kuchukuliwa na watu wenye taaluma ya uigizaji.

Watanzania msiwe na hofu kuhusu ndege- Kamwelwe
Alikiba ''siishi kistaa kama watu wanavyosema''