Mwanadada, msanii wa bongo Movie, mjasiliamali na  mwanamitindo maarufu aliyewahi kuwa mpenzi wa moja ya wasanii toka kundi la WCB Wasafi, Jackline Wolper ametoa mpya jana baada ya kufanya tukio la kihistoria ambalo halikuwahi kutegemewa na mtu yeyote.

Mwanamitindo Jackline Wolper ameingia kwenye orodha ya wasichana ambao wamewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Rajabu, maarufu kama Harmonize ambaye anafanya vizuri katika sanaa yake ya muziki.

Siku mbili zilizopita, Harmonize ameachia kibao chake akiwa amemshirikisha msanii toka Nigeria  Korede Belo ambaye wamefanya ngoma kali inayoitwa shulala, ngoma hiyo ikiwa inafanya vizuri katika mitandao ya kijamii hasa You tube.

Mara tu baada ya Harmoze kutoa ngoma hiyo, Wolper kwa kutumia ukurasa wake wa instagram ameupost wimbo huo na kuusindikiza na maneno mazuri yakuisifia kazi hiyo.

“Haka ka nyimbo kazuriii sana na video pia ndo usiseme!..bwana Raaaaaj umejua kunyoosha!Kama bado haujaangalia video ya haka ka wimbo pita kwenye bio ya @harmonize_tz
#Uliyemchokozakaja”. Ameandika Wolper

Jackline Wolper ambaye kwa sasa hayupo kimahusiano na Harmonize, toka waachane imepita miezi kadhaa, lakini wawili hao bado inasemekana hisia zao zipo pamoja.

Hilo linadhihirishwa wazi mara tu baada ya wawili hao kufarakana, Harmoze alikaa chini na kumuandikia mistari Wolper akionesha amechoka lakini ngoma hiyo ilitafsiriwa tofauti na mashabiki wa wapenzi hao.

 

 

 

 

Babu Seya amuomba JPM kupitia faili lake
Wasanii wasio na maadili kushughulikiwa