Msanii wa filamu nchini, Jackline Wolper amejibu swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza juu ya kurudiana na Harmonize kufuatia ujumbe mzito alioweka kwenye ukurasa wake ya Instagram siku ambayo Harmonize alizindua Album yake ya Afro East iliyuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu, wakiwemo viongozi wakubwa, wasanii wa muziki na filamu na watu mashuhuri.
Wolper amesema hawezi kurudiana na mtu ambaye waliachana akidai kuwa kwa sasa yupo ‘levo’ nyingine, Wolper pia amehoji “unamrudia mpenzi uliyeachana naye ili iweje”?.
”Mimi binafsi yangu sipo kwenye hizo levo za kurudia, unamrudia ex ili iweje sasa, kwanini kwamba huna mtu kwa wakati huo, au hauna mtu better kuliko yeye, waniache na maisha yangu ya ‘personal’ huwa na maamuzi magumu, mimi ni mkavu” Amesema Wolper.
Pia amezungumza kuwa katika vitu ambavyo hawezi kuvifanya ni kuongelea ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize akidai kuwa wawili hao wanajuana sana.
“Siwezi kuingolea ndoa ya Harmo, mimi tunajuana ananijua namjua, ukileta sumu hapa nimpe siwezi kumpa na yeye hawezi kunipa, kwahiyo tunajuana nyie hamjui jinsi mimi na yeye tunajuana, kahiyo mwanamke wake na shabiki zake watuachage sisi tuishi” Amesema Wolper.
Wolper amesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo na moja ya chombo cha habari alipokuwa anazindua duka lake la vitenge linaloenda kwa jina la muuza vitenge wa kishua ambapo amelazimika kufanya biashara hiyo kufuatia janga la corona linalotafuna watu duniani nzima, kwani lengo lake lilikuwa ni kufanya biashara kulingana na misimu mbalimbali, hivyo Corona imempelekea ashindwe kusafiri nje ya nchi kuchukua bidhaa hizo.
Na kuongeaza “Katika watu na vitu ambavyo watu wanatakiwa wajue ni kuhusu mimi na sara, yule sara umfate popote hawezi kuniongelea mimi vibaya sababu anaujua ukweli kuhusu mimi na mume wake, kwahiyo mimi binafsi yangu natakiwa labda hata Sara nimpe ushauri ni jinsi gani ya kuishi na mume wake, lakini mimi nimponde Sara kwenye intsgram trust me i will never do that”.
Aidha mjasiliamali huyo ametoa sababu zilizopelekea baadhi ya biasahara zake za nyuma kufeli ikiwemo ile ya ufundi cherehani akidai kuwa mwenye nyumba wake alimgeka kutokana na uzembe wake wa kutosaini mkataba wa nyumba hiyo.