Meneja wa FC Barcelona Xavier Hernández Creus amesema hawezi kutoa visingizio, baada ya kikosi chake kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano.
Kichapo hicho kimeifanya FC Barcelona kukosa nafasi ya kuongoza kwa tofauti ya alama 14 kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Hispania maarufu La Liga.
Barca wanatazamiwa kumaliza kusubiri kwao kwa miaka minne kutwaa taji la ligi katika majuma kadhaa yajayo, na kipigo cha mabao 4-2 cha Real Madrid dhidi ya Girona juzi Jumanne kiliwapa fursa ya kujiweka karibu zaidi na ufalme huo.
Hata hivyo, mabao ya Alvaro Garcia na Fran Garcia yaliipa Rayo ushindi unaostahili, huku bao la dakika za mwisho la Robert Lewandowski likionekana faraja tu kwenye mchezo huo wa juzi.
Barca wamepoteza michezo mitatu pekee za ligi msimu mzima, lakini Blaugrana hao sasa wamechukua pointi tano tu katika mechi 12 kwenye La Liga.