Kocha Mkuu wa FC Barcelona Xavi Hernandez amefichua siri kwamba anamkubali sana Alvaro Morata akisisitiza alizungumza na mshambuliaji huyo kuhusu uwezekano wa kumsajili.
Pia alifichua kuwa anampenda mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania na alitarajiwa kutua Camp Nou katika usajili wa uliopita lakini uhamisho wake ukabuma.
Kocha huyo alisema: “Kweli nilitaka kumsajili, nilitaka ajiunge na Barcelona, lakini haikuwezekana, nampenda sana Morata, ni mchezaji mkubwa, ana ukarimu na anafanya kazi kwa bidii, Atletico Madrid ina safu nzuri sana ya ushambuliaji.”
FC Barcelona iliripotiwa ilijaribu kumsajili Morata katika usajili wa mwezi Januari mwaka 2021 alipokuwa kwa mkopo Juventus akitokea Atletico Madrid, kwa mujibu wa ripoti.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alikuwa hapati nafasi nyingi za kucheza Juventus na alikuwa anafikiria kurejea Atletico licha ya kuhusiswa na Camp Nou.
Hata hivyo, Juventus ilikuwa haina nia ya kumtema Morata kipindi hicho na kutibua dili la FC Bracelona kumsajili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa na kiwango bora akiwa na kikosi cha Atletico msimu huu, akiwa amefunga mabao 12 katika mechi 17 michuano yote, pamoja na mabao saba ya La Liga sawa na Robert Lewandowski.