Aliyekuwa Kiungo wa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa jijini London ‘ Arsenal FC’, Granit Xhaka ameweka wazi uamuzi wa kuondoka kabla ya kumwagia misifa kocha wake Mikel Arteta.

Kiungo huyo ambaye mahusiano yake na mashabiki yalikuwa sio mazuri kipindi chote anakipiga Arsenal, lakini baadaye alikuwa mchezaji tegemeo kwenye kikosi msimu uliopita.

Akizungumza na gazeti la Marca, Xhaka amekiri alifanya uwamuzi mgumu alipoondoka Arsenal na kukiri amejiunga na Bayer Leverkusen asakae mapya mbali na Arsenal.

Xhaka alisema: “Nilidumu kwa muda wa miaka saba Arsenal, sikutaka kucheza dhidi ya Arsenal. Haikuwa rahisi kuondoka au klabu yenyewe kuniachia. Nawaheshimu sana bosi wangu Edu na Artea, lakini nilitaka kusaka changamoto nyingine Bayer Leverkusen.”

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswisi aliendelea kuzungumza kuhusu mahusiano yake na Arteta na kumfananisha na kocha wake wa sasa Xabi Alonso.

“Falsafa zao zinafanana sana, Arteta ni kocha mzuri na nafikiri Xabi anafuata nyayo hizo hizo. Wote wanautazama mchezo wa soka kwa jicho la tofauti,” aliongeza.

Xhaka ana matumaini ya kutoboa Bundesliga baada ya kutua katika dirisha hili la usajili la kiangazi na kuisaidia Bayer Leverkusen kwenye michuano ya Europa msimu ujao.

Bayer Leverkusen ilimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa Bundesliga msimu uliopita na Xabi ataingoza timu yake kwenye michuano ya Europa msimu ujao.

Arsenal ilisajili Declan Rice kama mbadala wa Xhaka akitokea West Ham kwa kitita cha 105 Pauni milioni, akifuatia na Kai Havertz.

Serikali yataka maoni marekebisho Sheria ya Madini
Young Africans yaanika ishu ya Mayele