Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amewataka wabunge kuendelea kusikiliza maoni mbalimbali yanayotolewa na wananchi kuhusu suala la uwekezaji Bandarini, lakini upande wa kuzungumza bungeni ulishapita na Bunge tayari lilimaliza kazi yake.

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 29, 2023, muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya wabunge ambapo amesema kuwa Bunge lilishamaliza mjadala huo, hivyo wabunge wanatakiwa kuendelea kuwasikiliza wananchi.

“Kuhusu suala la bandari tuendelee kuwasikiliza wananchi kwani sisi Bunge tulishamaliza kwa sehemu yetu, na kwa kuwa Bunge lilishafanya maamuzi yake basi wakati wetu ni pale tutakapohitaji mikataba iletwe bungeni ili tuipitie,” amesema Dkt. Tulia.

Kwa Mujibu wa Dk Tulia, watatumia hoja na maoni ya wananchi katika kuishauri Serikali utakapofika wakati huo lakini watatumia maoni na ushauri wa wananchi kwani kazi ya Bunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa maslahi ya wananchi.

Kikokotoo: Wabunge waanza upya Dodoma
Hesabu za CAG hazina mashaka - Mwigulu