Kama utakuwa umesahau au hufahamu basi Joseph Kibwetere aliwahi kuishangaza Afrika na Dunia kiujumla, yeye ni raia wa Uganda na alikuwa ni Mwalimu wa shule ya msingi.

Mara kadhaa alijiingiza katika harakati za siasa lakini akashindwa kuwashawishi Wananchi na kuuteka umma kwa sera zenye mashiko, hivyo akatafakari njia
nyingine ya kutoka akaona DINI itamlipa.

Kupitia kona hiyo gari la kibwetere likawaka, huko akawapumbaza watu kwa kujiita ‘Nabii na Mtume’ na kuwateka kwa maneno matamu na yenye ushawishi huku akitumia vibaya vifungu vya maandiko MATAKATIFU.

Kwa msisitizo na sura isiyo na shaka aliwaahidi Waumini wake kuwapeleka peponi, lakini mwisho wao ukawa mbaya kwani aliwauwa kwa kumwaga Petroli na kuwachoma moto akiwaaminisha kwamba mwisho wa dunia umefika.

Tukio hili ni baya kuwahi kutokea Barani Afrika, kwani aliwapa watu imani iliyojaa udanganyifu na kuacha majonzi makubwa huku yeye ikidaiwa kuwa alijificha na baadaye kutoroka.

Mzee wetu Jakaya Mrisho Kikwete (Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), aliwahi kunena kwamba, “akili za kuambiwa changanya na za kwako.”

Serikali, AZAKI ziimarishe uhuru wa Habari, taarifa - TAMWA-ZNZ
Muunganiko wapinzani, waasi waitikisa Serikali DRC