Habari kuhusu sheria mpya ya Eritrea ya kuwalazimisha wanaume kuoa wanawake wawili au zaidi na kwamba watakaokiuka amri hiyo watafungwa jela maisha, ilipata nafasi kwenye vyombo vingi vikubwa vya habari duniani, lakini habari hiyo imebainika kuwa sio ya kweli.

Chanzo kikuu cha uzushi wa habari hiyo kimebainika kuwa ni mtandao maarufu wa Kenya wa SDEKenya ambao umekuwa ukizusha habari nyingi na kuzitafutia nafasi kwenye vyombo vikubwa vya habari duniani.

Utafiti wa habari hiyo iliyoaminika kwa wengi, umebaini kuwa hakuna sheria mpya iliyotungwa hivi karibuni nchini Eritrea kuhusu mabadiliko ya sheria ya ndoa.

Sheria ya ndoa ya Eritrea hairuhusu mwanaume kuoa mwanamke zaidi ya mmoja na wanaokaidi amri hiyo hukumbana na kifungo cha hadi miezi 12 jela.

Tunaomba radhi kwa habari hiyo iliyoaminika kwa wengi duniani kote na kupelekea hadi waandishi wakubwa wa masuala ya haki za binadamu kuandika makala nzito kuhusu amri hiyo kwa imani kuwa imetungwa kweli.

Hivi ndivyo inavyosomeka sheria ya ndoa ya Eritrea:

Sheria ya Eritrea kuhusu NdoaSheria Eritrea 2

Mbowe aeleza watakachofanya kuzuia mpango wa Nape kuhusu TBC
Stephan El Shaarawy Aihama AC Milan