Mwandishi wa habari mkongwe wa Ujerumani aliyetajwa kwa jina la Jürgen Todenhöfer aliyewahi kutumia siku kumi nchini Syria na Iraq katika ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na kundi la kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq na Syria (ISIS), ametoa ripoti kuhusu nchi pekee ambayo kundi hilo linaiogopa.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Todenhöfer ambaye alikuwa nchini Syria mwaka 2014 na kupata nafasi adimu ya kutembelea miji kadhaa inayodhibitiwa na wapiganaji wa ISIS, kutembelea magereza ya wafungwa wanaoshikiliwa na kundi hilo, na wananchi wanaoishi chini ya utawala wa ISIS, alibaini ukweli uliojificha kuwa kundi hilo linaiogopa nchi ya Israel pekee kivita.

“Nchi pekee ambayo ISIS inaiogopa ni Israel. Waliniambia wanajua jeshi la Israel lina nguvu kubwa zaidi inayowazidi,” mwandishi huyo mkongwe aliuambia mtandao wa Jewish News.

Alisema kuwa ISIS hawaiogopi Marekani na Uingereza kwa kuwa wanajua vikosi vya ardhini vya nchi hizo havina uzoefu mkubwa wa kupigana vita vya msituni/ardhini au kukabiliana na ugaidi, lakini wanaamini Israel ina nguvu kubwa katika nyanja hiyo ya mapigano.

 

Hanspope Wa Simba Azushiwa Jambo Zito
Serikali Yawatoa Hofu Waganga wa Tiba Mbadala, Ni baada ya Kuwatangazia Marufuku