Kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso Yacouba Songne ameaga rasmi Ihefu SC, baada ya kukamilisha mpango wa kusajiliwa na Arta Solar 7 ya Djibout.

Yacouba alijiunga Ihefu FC wakati wa Dirisha Dogo la Usajili msimu uliopita akitokea Young Africans, na aliiisaidia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo ya mkoani Mbeya katika Kampeni zake za kutokushuka daraja.

Kiungo huyo aliyewahi kuitumikia Asante Kotoko ya Ghana ameaga Ihefu FC kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, akiandika maneno mazito na yenye faraja kwa Mashabiki, Uongozi na Wachezaji wenzake ambao amewaacha klabuni hapo.

Pia Yacouba amegusia namna alivyofurahishwa na maisha yake akiwa nchini Tanzania, ambapo kwa mara ya kwanza alisajiliwa Young Africans msimu wa 2020/21. Yacouba ameandika: “Ulikuwa wakati mzuri wa Kuishi Tanzania lakini pia ulikuwa wakati mzuri wa kuitumikia Ihefu napenda kuwashukuru wachezaji wote na benchi la ufundi wa Ihefu kwa kipindi chote tulichokuwa pamoja na niwatikie kila la kheri katika msimu huu mpya uwe ni msimu wenye mafanikio zaidi 🙏 SIKU ZOTE TANZANIA ITAISHI KWENYE MOYO WANGU.

Neymar kujimwambafai Saudi Arabia
Julio aitahadharisha Simba SC