Mshambuliaji kutoka Burkina Fasso Yacouba Sogne mwenye mabao saba katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara ‘VPL’ amewakosha viongozi wa klabu ya Young Africans kutokana na moto wake.

Sogne aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Asante Kotoko ya Ghana, ndiye mchezaji pekee wa Young Africans aliyefunga mabao mengi katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu msimu huu, jambo ambalo limekuwa gumzo miongoni mwa mashabiki, wanachama na viongozi wa klabu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Young Africans, Dominick Albinus amesema mshambuliaji huyo, ameonesha uwezo wake kwa kufunga mabao yanayoisaidia timu katika kipindi hiki, ambacho wanawania ubingwa wa Tanzania Bara, pamoja na kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

“Kuna watu wanaona kama hapa Young Africans hakuna Kamati ya Usajili sio sawa, muangalieni Yacouba. Sasa watu huko nyuma hawakuwa wanamuelewa kabisa na uwepo wa mabadiliko wa makocha msimu huu ukachagiza zaidi lakini huyu ni mshambuliaji aliyekamilika.”

“Bahati nzuri ni kwamba Yacouba alisaini mkataba wa miaka miwili na tutakuwa naye kwa msimu ujao ambao wengi wataona mengi zaidi ya ubora wa mshambuliaji huyu.”

“Kama kuna timu haijakutana naye basi kuanzia sasa wajiandae kwani gari ni kama ndio limewaka.” Amesema Albinus.

Gomes: Simba inanidai
Ndugai ambananisha Kalemani, awashukia Mawaziri