Kutoka kwenye ukurasa wa Dkt. Festo Ngadaya ✍?
Haya magonjwa pia uhusisha matamanio ya kingono ambapo mtu hupata hisia (hamu ya tendo) katika hali ambayo sio ya kawaida.
Zipo hali tofauti katika kundi hili. Acha tuanze kuzichunguza.
Fetishistic disorder au fetishism ni pale mtu anakua na hisia kali au matamanio ya kushiriki tendo na vitu visivyokua na uhai, mfano ni vitu kama midoli, viatu, nguo n.k au inaweza kuwa sehemu za mwili (mfano miguu, matiti, makalio)
Exhibitionistic Disorder au Exhibitionism ni ugonjwa wa afya ya akili ambapo mtu anakuwa na hamu ya kuonesha sehemu za siri za mtu mwingine aidha kwa kupiga picha na kurusha kwa umma (public) au hata kumvua mtu hadharani ili watu wote waone.
Frotteurism yenyewe mtu huwa na hisia kali, matamanio yasiyo ya kawaida au tabia ya kujiridhisha mwenyewe kwa kujishika au kusugua sehemu za siri dhidi ya kitu fulani (sio kama wanavyofanya wanaosagana), hapa inakua dhidi ya object mfano sink la choo, benchi la kukalia, mto n.k
Sexual mesochism disorder, ni hali ambapo mtu hupandisha hisia pale tu anapofanyiwa kitendo fulani mfano kwa kupata maumivu fulani kama kupigwa, kuteswa au muda mwingine hata kudharirishwa yeye ndio hisia zinapanda.
- Spanking au whipping (kupigwa makofi makalioni au mijeledi)
Voyeuristic disorder mtu anakuwa na matamanio ya kuona wengine ama wakiwa uchi au wanashiriki tendo, hawa ni wale wazee wa chabo.
Chabo ni ugonjwa wa afya ya akili, yani raha yake ni kuona watu wakiwa wanafanya yao, au wanavua nguo, wanaoga ili aone tu utupu wa mwingine.
Pedophilia au pedophilic disorder, hawa sio wageni katika jamii, ni pale mtu mzima anavutiwa kingono na watoto wadogo.
- Mtu mzima anapandwa na hisia za kingono akimuona mtoto mdogo.
Sexual Sadism Disorder ni pale mtu ili apandishe hisia ni lazima asababishe maumivu, amtese au kumdharirisha mtu mwingine.
Zipo nyingine kama coprophilia (unavutiwa na kinyesi), necrophilia (unavutiwa kufanya mapenzi na maiti), urophilia (unavutiwa na mkojo wa mtu), au kuvutiwa kushiriki tendo na wanyama (zoophilia).
Bila shaka umeliona kundi la changamoto ya afya ya akili unayomiliki.