Mchezo wa kundi ‘E’ kati ya Brazil na Costa Rica umemalizika kwa Brazil kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dakika za lala salama.

Wakati mashabiki na wachezaji wa Brazil wakidhani jahazi lao linaenda kuzama dakika 6 za nyongeza zimetosha kuwamaliza Costa Rica ambapo Philepe Coutinho aliwainua mashabiki wa Brazil kwa kupachika bao kabla ya Neymar kumalizia kalamu ya mabao kwa kupachika bao la pili sekunde chahe kabla ya mchezo huo kumalizika.

Nusra Brazil wapate suluhu ya pili kwani Costa Rica licha ya lango lao kushambuliwa walicheza kwa kujilinda mpaka dakika ya 90 matokeo yakiwa 0-0.

Kwa matokeo hayo Brazil ndio vinara wa kundi ‘E’ wakiwa wanaongoza kwa jumla ya pointi 4 baada ya kushuka dimbani mara mbili. Serbia wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 3 huku Switzealand wakiwa na point moja na Costa Rica wakiburuza mkia wa pointi 0.

Kiungo wa Brazil Casemiro akitibiwa baada ya kupigwa na mpira puani na kuanza kuvuja damu

 

 

Serikali yatoa tamko la tozo ya daraja la kigamboni
China kuadhimisha tamasha la ulaji nyama ya mbwa