Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha utoaji huduma za utangazaji kwa Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba jijini Dar es Salaam ambapo amesema hatua hiyo ni kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018.

Mhandisi Kilaba amesema kuwa ukiukwaji huo wa kanuni ulifanyika katika vipindi vya The Switch na Mashamsham.

Aidha, ametoa rai kwa vyombo vya habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania huku akiitaka Wasafi FM kuomba radhi kwa umma wa Watanzania.

NEMC: halmashauri fanyeni utafiti wa taka
Kubenea aachiwa huru kwa dhamana