Klabu ya Azam FC imemsajili Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, kwa mkataba wa miaka miwili.
Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu yetu hadi mwaka 2023.
Kabla ya kutua Azam FC Mbombo alikua akiitumikia klabu ya El Gouna ya Misri.
Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors (zote za Zambia), anakwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Azam FC.
Huo unakuwa usajili wa tano kwa Azam FC kwenye dirisha hili, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao, awali waliwasajili nyota watatu kutoka Zambia, Charles Zulu, Paul Katema, mshambuliaji Rodgers Kola na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.