Kocha mzawa, Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika  Machi 31, 2017.

TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.

Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.

Naye kocha Mkwasa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.

Aidha, Kocha Mkwasa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Mkwasa amesema kikosi chake kipo kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya DRC.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa kesho” Alisema Mkwasa.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.

 

Stars Kuanza Kusaka Tiketi Ya Urusi Kesho
Sir Alex Ferguson Aendelea Kutetea Uamuzi Wake