Mshambulaijij kutoka Burkina Faso Yacouba Sogne, amekamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Young Africans, na anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote tayari kuungana na wachezaji wengine kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligu Kuu 2020/21.

Sogne anakua mchezaji wa kwanza wa kigeni kudhihirishwa na uongozi wa klabu ya Young Africans, baada ya wachezaji wazawa kuendelea kusajiliwa klabuni hapo na kutambulishwa kila kukicha.

Mshambuliaji huyo anaejiunga na Young Africans akitokea Asente Kotoko ya Ghana, amesaini dili la miaka miwili.

Sogne amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi cha Young Africans ambacho anaamini ni njia yake ya kufikia mafanikio.

Gwambina FC, Namungo FC zapigana vikumbo kwa Yondani, Juma
Papaa Zahera kocha mkuu Gwambina FC

Comments

comments