Mshambuliaji mzimbabwe wa Yanga Donald Ngoma atahitaji mapumziko ya wiki moja kabla ya kurejea tena mazoezini kuumia katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara VPL dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ngoma aliondoka uwanjani akiwa anachechemea dakika ya 77 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi ambapo Yanga ililazimishwa sare ya kutofungana na Mtibwa katika mchezo wa ligi kuu ya VPL uliopigwa siku ya Jumamosi.
Baada ya mchezo huo Ngoma alipimwa na kugundulika kuwa misuri ya ndani ya paja ilivutika siku hiyo na kumsababishia maumivu kwa mujibu wa Daktari wa Yanga Edward Bavu.
-
Simba yaapa kutokutoka Kileleni
-
Donald Ngoma aiweka roho juu Young Africans
-
Kocha wa Azam FC kuwatupia jicho Azam B
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa maiaka 28 raia wa Zimbabwe, amekuwa alijiunga na klabu ya Yanga mwaka 2015 na amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu.
Mpaka sasa Yanga wanashika nafasi ya 6 katika ligi kuu ya soka ya Tanzania bara wakiwa wamecheza michezo mitano na kukusanya jumla ya pointi 9 wakati watani wao wa jadi Simaba wakiongoza msimamo wa ligi kuu kwa pointi 11.