Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna mchezaji wa kumlinganisha na Emmanuel Okwi, Afrika Mashariki kwa sasa kwani yupo katika kiwango cha juu japo timu ya Yanga walicheka kipindi cha usajili huku wakimuita jina la muhenga.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba kuanza vizuri katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifungia mabao sita timu yake,katika mechi mbili na kuweza kuzima maneno ya wapinzani wao waliyokuwa wanamuita muhenga kipindi alipokuwa akisajiliwa.

“Afrika Mashariki ina Okwi mmoja tu, michezo miwili goli sita, mara mbili ya magoli yote ya Yanga kwa michezo yao mitatu, kosa lao lilikuwa kumuita muhenga, atashinda kila tuzo nchi hii, hii ni Simba na huyo ndiyo Okwinho,” ameandika Manara

Hata hivyo, klabu ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza Septemba 21 mwaka huu dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa mzunguko wa nne wa Ligi Kuu Tanzania Bara

 

Ukimwi wazidi kuwa tishio nchini
Video: Hivi ndivyo Lukaku alivyoiliza Everton