Afisa habari wa Yanga sc Hassan Bumbuli amesema kwenye ratiba yao wanatambua kuwa wamebaki na michezo (4) pekee.

Ameongeza kusema kuwa jumapili hii klabu ya Yanga itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon Chamanzi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zinadai, uongozi wa Yanga sc ulipokutana na TFF uliiambia kuwa kucheza mchezo huo ni kuvunja kanuni hivyo basi wakaombwa watumie busara.

Baada ya kuombwa watumie busara klabu hiyo pia ikaiomba TFF nao watumie busara kuhusu suala la makamu mwenyekiti wa Yanga aliyefungiwa miaka (5) asijihusishe na soka Fredrick Mwakalebela,, TFF ikakataa.

Ndipo Yanga nao wakakataa pia kucheza mchezo huo kwa madai kuwa ni kuvunja kanuni ambazo wanazisimamia (TFF).

Nabi: Yanga itakua tishio Afrika
Shikalo kurudi Kenya