Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga, wataanza na St Louis ya Shelisheli katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano ugenini.

Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.

Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.

Na ikivuka hatua hiyo, Yanga itakutana na mshindi kati ya Township Rollers ya Botswana na El Merreikh ya Sudan.

Timu tano hazijapangwa katika hagtua ya awali, ambazo ni Al Ahly ya Misri, mabingwa watetezu, Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwa upande wa Wekundu Wa Msimbazi Simba wataanza na Gendarmerie Tnale ya Djibouti katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano ugenini.

Simba Ikivuka hatua hiyo, itakutana na mshindi kati ya El Masry ya Misri na Green Bufaloes ya Zambia.

Magereza wazungumzia msamaha wa 'Lulu'
Mshindi wa kura za maoni CCM atiwa mbaroni