KMKM ya Zanzibar na Yanga SC hatimaye zimefikia makubalino juu ya mlinda mlango Mudathir Khamis.

Kipa huyo namba Zanzibar alimalizana na Yanga SC mwezi uliopita, lakini klabu yake, KMKM ikaweka ngumu hivyo akashindwa kujiunga na timu yake mpya.

Lakini leo, Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha amesema suala hilo limemalizwa.

“Sisi na KMKM tumemalizana kiungwana juu ya kipa huyu (Mudathir). Sasa naweza kusema Mudathir yuko huru kujiunga na Yanga SC kwa Mkataba wa miaka miwili,”amesema Dk. Tiboroha, ambaye utendaji wake unawafurahisha wana Yanga wengi.

Mudathir sasa atajiunga na kambi ya Yanga SC inayojiandaa na michauno ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, inayotarajiwa kuanza Jumamosi, Dar es Salaam.

Azam FC Watimiza Ndoto Za Kumsajili Mshambuliaji Wa Kinyarwanda
Man City Wamaliza Mzizi Wa Fitna, Wamsajili Rasmi Sterling
Tags