Klabu ya Fountain Gates imetangaza kuvunja benchila ufundi lililokuwa linaloongozwa na kocha Mohammed Muya. Maamuzi ya kuivunja benchi hilo yamefanywa na Uongozi wa timu hiyo na sababu kubwa ni kupoteza mchezo kwa mabao 5-0 dhidi ya Yanga .
Katika mchezo huo Yanga walijipatia mabao mawili kupitia Pacome Zouzoua dakika ya 16 na 45.Mabao mengine yalifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 41 na Clement Mzeze dakika ya 88.Shiga wa Fountain Gates alijifunga bao dakika ya 52.
Je ni Sahihi kwa Fountain Gates kulivunja benchi la Ufundi
Mwenendo wa Fountain Gates umekuwa mbaya tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba baada ya kufungwa mabao 3-1 na pamba jiji,Kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania,kufungwa 2-0 na Azam ,kufungwa 2-1 na Namungo fc na sasa 5-0 dhidi ya Yanga .
Fountain gates wameshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Coastal Union (3-2) katika michezo 6 waliyocheza hivi karibuni. Klabu hiyo chini ya kocha Mohammed Muya walifungwa jumla ya mabao 13 na kufunga mabao 3 pekee katika mechi hizo 6 za mwisho na walivuna alama tatu pekee.
Kwa sasa Fountain Gates iko nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 20 tofauti ya alama 5 na Tabora United walio nafasi ya 5 wakiwa na mchezo mkononi.
Barua ya Uongozi wa Fountain Gates