Timu ya Ruvu Shooting imevunja mwiko kwa kuichapa klabu ya Yanga bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Vodacom uliomalizika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Bao pekee na Ruvu Shooting limewekwa kimiani na Sadat Mohamed akimvisha kanzu kipa wa Yanga, Farouk Shikalo mnamo dakika ya 20 kipindi cha kwanza.

Aidha, bao hilo limeweza kudumu kwa dakika zote 90 ambapo mpaka Mwamuzi, Martin Saanya alipohitimisha mchezo huo kwa kupuliza kipyenga cha mwisho, ubao ulikuwa unasomeka bao 1-0.

Katika mechi hiyo, Kocha Mwinyi Zahera aliwatoa nje wachezaji, Sadney Urikhob na kumwingiza Maybin Kalengo, Juma Balinya akimtoa pia na nafasi yake akichukua Balama Mapinduzi lakini mabadiliko hayakuleta mafanikio.

Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia kuendelea hapo kesho ambapo bingwa Mtetezi Klabu ya Simba itashuka dimbani kucheza na Polisi Tanzania katika uwanja wa Uhuru.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 29, 2019
RC Makonda aja na hoja ya marekebisho ya sheria ya Ndoa