Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC, wameichapa timu ya Stand United magoli 3- 1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa
Mabao ya Yanga yamefungwa na mlinzi wa Stand United Ally Ally ambaye alijifunga dakika ya 7 kabla ya mshambuliaji Ibrahim Ajib kufunga bao la pili dakika ya 12 na Obrey Chirwa kufunga dakika ya 85, huku bao pekee la Stand likifungwa na Vitalis Mayanga.
Aidha, timu zingine saba ambazo Yanga imezifunga mfululizo ni Ruvu Shooting, Azam FC, Lipuli FC, Njombe Mji FC, Majimaji FC, Ndanda FC na Kagera Sugar FC. Baada ya kushisnda mechi hizo Yanga imefanikiwa kumaliza tofauti ya alama 8 na Simba zilizokuwepo mwezi Desemba.
Hata hivyo, ushindi wa leo umeifanya Yanga kufikisha alama 46 sawa na vinara Simba wenye alama 46, huku Yanga wakiwa na mechi 21 na Simba wakiwa wamecheza mechi 20. Simba inasalia kileleni ikiwa na mabao mengi zaidi ya Yanga. Simba wana mabao 38, Yanga wakiwanayo 28