Mabingwa wa ligi kuu nchini timu ya Yanga itaindikia barua Bodi ya ligi (TPLB) ili kusogeza baadhi ya mechi mbele kutokana na kukaribiana huku miundo mbinu ya usafiri ikiwa sio rafiki.

Yanga imesonga mbele katika hatua ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa St Louis ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1 na imerejea nchini usiku wa jana ikitokea visiwani humo.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema wachezaji wamepumzika leo na kesho watasafiri kuelekea Songea kwa ajili ya mchezo wa FA dhidi ya Majimaji siku ya Jumapili.

Mkwasa amesema baada ya mchezo wa Majimaji timu itasafiri kwenda mkoani Mtwara kucheza mechi ya ligi dhidi ya Ndanda kabla ya kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa na kurejea jijini Dar es Salaam kukutana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika.

“Ratiba ni ngumu wachezaji hawana muda wa kupumzika tunacheza mechi mfululizo, tutaiandikia barua Bodi ya ligi ili kuangalia watatusaidiaje katika hili. Tunasafiri umbali mrefu na miundo mbinu ya barabara zetu sio rafiki sana” alisema Mkwasa.

Licha ya ratiba hiyo kubana Yanga pia inaandamwa na idadi kubwa ya majeruhi ya wachezaji wake nyota.

Taarifa kutoka RT, wakubali agizo la BMT
Mwingine abainika kutumia dawa haramu michezoni