Klabu ya soka ya Yanga kesho inatarajia kumjua mpinzani wake kwenye mchezo wa mtoano wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika kupitia droo itakayochezeshwa na CAF.
Droo ya ratiba ya mechi hizo za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho itapangwa makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yaliyopo jijini Cairo nchini Misri.
Aidha, Timu ambazo zipo kwenye droo hiyo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika Kusini na Al-Hilal Al-Ubayyid ya Sudan.
Zile zilizotoka kwenye ligi ya Mabingwa na kudondokea Shirikisho ni AS Vita ya DR Congo, ASEC Mimosas, Williamsville AC za Ivory Coast, Saint George ya Ethiopia, CF Mounana ya Gabon, Aduana Stars ya Ghana, Gor Mahia ya Kenya na UD Songo ya Msumbiji.
-
Kikwete: Viongozi Simba SC, Young Africans mjitathmini
-
Azam FC kujipima kabla ya kuwavaa Mtibwa Sugar
-
Hotuba ya Rais wa TFF alipozungumza na wahariri wa habari za michezo Jumatatu Machi 19-2018
Zingine ni MFM, Plateau United za Nigeria, Rayon Sports ya Rwanda, Generation Foot ya Senegal, Bidvest Wits ya Afrika Kusini, Al-Hilal ya Sudan na Zanaco ya Zambia. Yanga imetolewa na Township Rollers ya Botswana kwa jumla ya mabao 2-1