Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ukipinga uamauzi wa Bodi ya Ligi kumfungia kocha wake Mwinyi Zahera mechi tatu kutokana na shutuma alizotoa kwa bodi hiyo baada ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting wakidai kuwa adhabu hiyo ni kubwa sana na haki haijatendeka.

Ambapo katika mechi hiyo Ruvu Shooting waliibuka kidedea baada ya kuitandika Yanga gori moja katika dakika ya 21 kupitia kiungo wao, Sadat Mohamed na kuwafanya Yanga kushindwa kurudisha gori hilo hadi mchezo kukamilika kwa matokeo ya 1-0.

Kufuatia matokeo hayo ya Ligi kuu kwenye mechi ya kwanza, Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alijikuta akiilalamikia Bodi ya Ligi hiyo kwa kukataa kusogeza mbele siku mbili mechi hiyo ili wachezaji wake wapate muda wa kupumzika baada ya mechi kubwa waliocheza kwenye mchuano mkali wa marudiano dhidi ya Township Rollers na kuibuka na ushindi wa 2-1 na matokeo hayo kuifanya Yanga kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema adhabu ya kufungiwa kocha mechi tatu ni kubwa sana na kushauriana kuwa ni bora angepigwa faini.

”Unapomfungia kocha mechi tatu kwa nini usimpe faini tu aendelee kufundisha timu? amehoji Mwakalebela.

Hivyo ameongezea kuwa tayari wameshaandika  barua Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ukipinga uamauzi na sasa wanasubiri majibu.

Fid Q asusia tamasha la Afrika Kusini
Tanzania, Uganda zaingia mkataba kujiinua kiuchumi